Mawaziri wa nchi wanachama wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki wanaohusika na usalama wameazimia kwa pamoja kuwa
na sera na sheria zenye tafsiri ya pamoja katika kusimamia baadhi ya masuala
yanayohusu usalama wa nchi hizo
Maazimio hayo yamefikiwa jijini
Arusha yalipo makao makuu ya EAC na Mawaziri hao katika kikao cha kisekta
ambapo kwa upande wa Tanzania waziri mwenye dhamana ya mambo ya ndani Dakta
Mwigulu Nchemba anasema miongoni mwa maazimio yaliyopelekwa na Tanzania ni
pamoja na kuwa na tafsiri moja kwenye suala la dawa za kulevya.
|
|
Kumekua pia na ongezeko la
biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu katika nchi za ukanda wa Afrika
Mashariki, hili nalo limewekwa kwenye maazimio hayo ambayo yanatarajiwa kufikiwa
maamuzi kwenye kikao cha wakuu wa nchi mwezi Novemba.
|
Nchi za EAC kuwa na Sheria na sera zenye taf siri moja
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 26, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment