WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameshiriki maziko ya aliyekuwa
mtumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu marehemu Bw. Atufigwege Mwakasege
yaliyofanyika katika makaburi ya Kikuyu mjini Dodoma.
Bw. Mwakasege ambaye
alihamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu Februari 29, 2016 akitokea Ofisi ya
Rais-TAMISEMI amefariki dunia Aprili 23 mwaka huu katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili ambako alikuwa amelazwa baada ya kuugua.
Akizungumza kwa niaba ya
Waziri Mkuu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,
Bunge, Vijana, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Bibi Jenista Mhagama amesema
kifo hicho kimeiachia pengo kubwa kwa Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na
familia.
“Natumia fursa hii kutoa pole
kwa wanafamilia hususan mjane na watoto. Marehemu ameacha pengo ndani ya
familia, hivyo tumuombe Mwenyezi Mungu awape uwezo na nguvu ya kuweza kuhimili
pengo hilo.”
Marehemu Bw. Mwakasege ambaye
alizaliwa Desemba 25, 1959 katika kitongoji cha Mwanjelwa mkoani Mbeya, ameacha
mjane Bibi Judith Mwakasege pamoja na watoto wane ambao ni Henry, Joel, Eva na
Kelvin Mwakasege.
Maziko hayo pia yamehudhuriwa na
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mama Mary Majaliwa, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera na Uratibu) Profesa Faustine Kamuzola, Katibu
Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Bi. Maimuna Tarishi, Watumishi wa
Ofisi ya Waziri Mkuu.
WAZIRI MKUU ASHIRIKI MAZIKO YA MTUMISHI WA OFISI YA WAZIRI MKUU
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 25, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment