Ugonjwa wa malaria kwa Mkoa wa Arusha umepungua na kuwa chini ya
asilimia Moja ambapo kwa mwaka 2017 wagonjwa wamepungua kutoka elfu kumi na
tano na mia Moja hamsini hadi kufikia elfu nne mia tatu thelathini
na tano sawa na punguzo la asilinia 71.
Hayo yamesemwa na mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha DOKTA Timothy
Onanji wakati akiongea na waandishi wa habari katika maadhimisho ya Siku ya
malaria duniani yaliyofanyika kimkoa sambamba na uzinduzi wa chanjo ya saratani
ya mlango wa kizazi ambapo amesema mafanikio hayo yametokana na jitihada
zilizofanyika ikiwemo matumizi ya vyandarua pamoja na utokomezaji wa mazalia ya
mbu.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Arusha Fabian Daqquro amesema
kuwa mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria bado yanahitajika hasa wakati huu
mvua zinapoendelea kunyesha hivyo wananchi wajitahidi kutumia vyandarua pamoja
na kuondoa mazalia ya mbu katika maeneo yao.
Naye mratibu wa Malaria Mkoa wa Arusha Dokta Sixter Komba
ameeleza kuwa ugonjwa huo umepungua kutokana na mikakati waliojiwekea
ambayo ni pamoja na upatikanaji wa dawa mseto, ugawaji wa
vyandarua pamoja na kuuwa viluilui vya mbu katika wilaya zote saba
za Mkoa wa Arusha.
Hata hiyo maadhimisho hayo yamefanyika kitaifa Mkoani
Kigoma umebeba kauli mbiu isemayo " Niko tayari kutokomeza malaria na wewe
je? "
TAKWIMU YA HALI YA UGONJWA WA MALERIA MKOA WA ARUSHA YAPUNGUA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 25, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment