Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kupitia baadhi ya wabunge wake, wameibua tuhuma nzito juu
ya tabia chafu inayofanywa na wamiliki wa majumba yanayotumika kutibu
waathirika wa madawa ya kulevya (sober house), kitendo kinachozidi kuwaathiri
vijana wakiwa humo.
Akizungumza Bungeni kutaka maelezeo
kutoka kwa serikali inachukua hatua gani juu ya hilo, Mbunge Kijana Halima
Bulembo amesema kwamba wamili wa majumba hayo wana tabia ya kuwachoma tena
sindano za madawa ya kulevya vijana ambao wanakaribia kupone ili wasitoke, na
lengo kubwa likiwa ni kuendelea kuingiza pesa kupitria wao.
“Kumekuwa na malalamiko mengi ya
waathirika wa madawa ya kulevya wanapokuwa rehab, wanapokaribia kupona wahusika
wanawachoma dawa tena za madawa ya kulevya ili wasiweze kutoka lengo likiwa
waendelee kijipatia fedha”, amesema
Halima Bulembo.
Taarifa hiyo iligongewa msumari na
Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama, kwa
kusema kwamba malalamiko hayo sio mara ya kwanza Bungeni, na kutoa onyo kali
kwa wamiliki.
“Tumepokea hii taarifa sasa
kwa mara kadhaa, waheshimiwa wabunge wametuarifu kwamba upo mchezo mchafu
unaoendelea kwenye sober house, badala ya kuwasaidia vijana wetu wapone, na
waondoke sober house, lakini wamiliki wanataka kuendelea kuwaweka pale kwa
faida yao binafsi. Nitoe agizo kwa wamiliki wa sober house ambao wana mchezo
huo kuacha haraka, na naagiza mamlaka husika kufanya uchunguzi wa kina na
yeyote atakayebainika kufanya jambo hilo tutamchukulia hatua kali”, amesema
Waziri Jenista Mhagama.
Kwa upande wa serikali wamesema
hawajapokea taarifa hizo rasmi kwa sababu asilimia kubwa ya sober house
zinamilikiwa na watu binafsi, lakini imeweka miongozo kusaidia soiber house, na
kuhakikisha kuwa mpango wa serikali kuwa na sober house nyingi inazomiliki
unafanikiwa ili kuondokana nalo.
Bunge laibua mazito yanayofanyika 'sober house'
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 25, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment