Jaji Mkuu wa Tanzania,
Profesa Ibrahim Juma amefunguka na kuweka wazi kuwa endapo viongozi wa Chama
Cha Wanasheria Nchini (TLS) watajiingiza kwenye masuala ya siasa na haraka
hivyo wao hawataweza kushirikiana nao kwa kuwa sheria zinataka kutojihusisha na
siasa.
Jaji Mkuu amesema hayo alipokuwa
akiongea na waandishi wa habari na kuwataka viongozi wa chama hicho kuendesha
shughuli zao kwa manufaa ya Umma kwani ikiwa vinginevyo watakosa ushirikiano na
vyombo vingine vilivyopo chini yake.
"Viongozi wanaoendesha chama
cha wanasheria Tanganyika (TLS) waendeshe gari lao kwa manufaa ya Umma
wasikubali kuingia kwenye harakati na siasa kwani wakifanya hivyo wale ambao
wanatakiwa kushirikiana nao hawatawapa ushirikiano, hivyo ukiingia kwenye siasa
wengine sisi tumekatazwa kuingia kwenye mambo ya siasa hivyo hatutashirikiana
na wewe"alisisitiza
Hata hivyo Rais wa Tanganyika Law
Society (TLS), Bi. Fatma Karume akiwa kwenye kipindi cha East Africa Breakfast
cha East Africa Radio aliweka wazi kuwa hana mpango wa kuingia kwenye siasa
lakini amedai hawezi kuacha kuikosoa serikali pale anapoona inavunja sheria na
kufanya mambo kinyume na kudai kwa hilo hataogopa kusema hata kidogo.
“I like my freedom, napenda kufanya
vile ninavyoona mimi, kama serikali inafanya vitu kinyume na sheria nitasema
kwamba hivi sio vizuri, si vizuri kuvunjia watu majumba yao wakati kuna court
order, nitasema sitaogopa, ila sitaki kugombea, sitaki siasa, I like to be left
alone”, amesema Fatma Karume.
"Hatutashirikiana na wewe" - Jaji Mkuu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 25, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment