Mbunge wa Ulanga (CCM), Goodluck
Mlinga amesema ndege aina ya Airbus 380, EK701 ya Shirika la Ndege ya Emirates
si ya kwanza yenye ukubwa huo kutua nchini kama inavyodaiwa na baadhi ya watu
Akizungumza katika mjadala wa
bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano mwaka 2018/19, Mlinga
amesema ndege ya kwanza kubwa kutua nchini ni aina ya Antonov mwaka 2009 ikiwa
imepakia mitambo ya kufua umeme ya Richmond
“Iliyokuja kipindi kile (Antonov)
ilikuwa na uzito tani 285 wakati hii iliyokuja jana ina tani 276. Iliyokuja
kipindi kile ilikuwa na injini sita, ila hii iliyotua jana ina injini nne.
Ndege hii iliyoleta mitambo ya Richmond ilikuwa na urefu wa mita 88 ila
hii ya jana ina mita 73,” amesema Mlinga
Mbunge ataja ndege ya kwanza kubwa kutua Dar
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 25, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment