Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imetakiwa kuisimamia
mitandao ya simu za mkononi inayopeleka huduma za Teknolojia za Habari na
Mawasiliano (Tehama) shuleni ili kuepusha kupeleka huduma hiyo eneo moja
Rai hiyo imetolewa leo Aprili 25 na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Uchukuzi na Mawasiliano, Dk Ave Maria Semakafu wakati wa maadhimisho ya
kimataifa ya Tehama ya mtoto wa kike inayofanyika kila mwaka Aprili 25
Dk Semakafu amesema kampuni zimekuwa zikijikita eneo moja na
wakati mwingine shule moja, huku mahitaji ya huduma hiyo ni makubwa hususan
katika shule zilizopo vijijini
"Yaani kuna wakati unakuta shule moja, vodacom,aitrl, tigo
wote wapo hapo kisa tu shule hiyo ipo mjini wakati wengine wanhgeweza kwenda
kwingine, hebu TCRA zisimamieni kampuni hizi ili kileta tija,” amesema katibu
huyo
Kuhusu siku ya Tehama kwa watoto wa kike, amesema itumike katika
kujitafakari nini cha kufanya kupitia teknolojia mbalimbali zinazovumbuliwa
kufikia Tanzania ya Viwanda
Awali, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Raymond Mfutahema amesema
katika siku hiyo pia pamoja na shughuli nyingine wamegawa vitabu 36 vya
muongozo wa matumizi ya mitandao uliotolewa hivi karibuni
Mbali na shule pia amesema wameshasambaza nakala zake 16,000
katika maeneo mbalimbali ya nchi ambayo itasaidia watu kusoma sheria hizo na
kuepuka kuingia katika mitandao.
TCRA yatwishwa jukumu kampuni za mitandao shuleni
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 25, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment