Rais John
Magufuli ametoa msamaha kwa wafungwa 3,319 katika kuadhimisha miaka 54 ya
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Katibu Mkuu,
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Projest Rwegasira katika taarifa kwa umma
iliyotolewa jana amesema wafungwa 585 kati ya waliosamehewa wangeachiwa huru
jana na 2,734 watabaki gerezani kumalizia sehemu ya kifungo kilichobaki
“Ni mategemeo
ya Serikali kwamba watarejea tena katika jamii kushirikiana na wenzao katika
ujenzi wa Taifa na kwamba, watajiepusha kutenda makosa ili wasirejee tena
gerezani,” anasema Rwegasira katika taarifa hiyo
Hata hivyo,
msamaha wa Rais hautayahusu makundi 21 ya wafungwa wakiwamo waliopatikana na
hatia na kuhukumiwa kwa kosa la kuzuia watoto kupata masomo
Mwanaharakati
wa kupinga ndoa za utotoni nchini, Rebeca Gyumi alipotakiwa maoni yake kuhusu
kutopata msamaha waliozuia watoto kupata masomo alisema ni jambo linalotafsiri
msisitizo wa elimu kwa mtoto nchini
Rebeca ambaye
ni mkurugenzi wa taasisi ya Msichana Initiative alisema hatua hiyo ni chachu
kwa mtoto kuendelea na masomo
Wafungwa
waliopewa msamaha na Rais kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya Ibara ya
45(1)(d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ni wote wanaopunguziwa robo ya adhabu
zao baada ya punguzo la kawaida la moja ya tatu linalotolewa chini ya kifungu
49(1) cha Sheria ya Magereza Sura ya 58
Wafungwa hao
sharti wawe wametumikia robo ya adhabu zao gerezani isipokuwa walioorodheshwa
katika ibara ya 2(i – xxi), ambao baadhi ni waliohukumiwa adhabu ya kunyongwa
au kwa makosa ya kujaribu kuua; waliohukumiwa kunyongwa na adhabu hiyo
kubadilishwa kuwa kifungo cha maisha au kifungo gerezani; na waliohukumiwa
kifungo cha maisha gerezani
Wengine ni
wanaotumikia kifungo kwa makosa ya kujihusisha na usafirishaji na matumizi ya
dawa za kulevya.
Wafungwa 3,319 wasamehewa, 585 watolewa jela
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 27, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment