Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) Mkoa wa
Mbeya, George Titho amekamatwa na polisi usiku wa manane nyumbani kwake
kijijini Kyimo wilayani Rungwe
Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Mussa Taibu
alipoulizwa kuhusu kukamatwa kiongozi huyo, amesema hana taarifa
"Sina taarifa hizo, labda nifuatilie lakini jua tu kwamba
hali Mbeya ni shwari," amesema Kamanda Taibu
Katibu wa Chadema Mkoa wa Mbeya, Boid Mwabulanga amesema
Titho alikamatwa usiku wa kuamkia Aprili 26, 2018
Mwabulanga amesema hawajaambiwa sababu za kukamatwa kwa
Titho na jitihada za kumwekea dhamana zimegonga mwamba
"Walikwenda nyumbani kwake saa nane usiku na kuvunja
mlango, wakachukua simu zake kisha wakamchukua kwenda naye kituo cha polisi
Tukuyu. Tumekwenda asubuhi kumwekea dhamana lakini walikataa,” amesema
Mwenyekiti wa Bavicha Mbeya akamatwa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 27, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment