Kikao cha Baraza la Madiwani wa
Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe Mkoani Mwanza kimevunjika baada ya Mkurugenzi
mtendaji wa halmashauri hiyo na wataalamu wake kususia kikao hicho kwa kile
kinachodaiwa kuwa sheria, kanuni na taratibu za kikao hicho zimekiukwa.
Hayo yamejiri kwenye kikao cha
Baraza la Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Ukerewe cha robo ya pili ya
mwaka ,ambacho kimeshindwa kuendelea na majadiliano mara baada ya madiwani
katika kikao hicho kuwasilisha hoja ya ukusanyaji wa mapato na ucheleweshaji wa
vikao lijadiliwe kama suala la dharura ndani ya kikao hicho.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri
hiyo Bw. Frank Bahari amesema kwamba Mwenyekiti wa halmashauri hiyo George
Nyamahakwa kushinikiza kuendelea na kikao hicho ni kukiuka sheria kanuni na
taratibu.
Hatua hiyo imechangia Mkurugenzi wa
Halmashauri hiyo pamoja na wataalamu wa halmashauri hiyo kutoka nje na kususia
kikao hicho wakidai kutoridhishwa na hali ya uendeshaji wa kikao hicho.
Kutokana na malumbano hayo yanayoathiri
maendeleo ya wananchi wa halmashauri hiyo Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Frank
Bahati amesema malumbano ya muda mrefu yatafanya halmshauri kushindwa kupanga
mipango ya maendeleo kama hawatokubaliana.
Aidha Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo
amedai kuwa malumbano hayo ya muda mrefu ndani ya halmashauri hiyo yamekuwa
yakiwaadhibu wananchi wao na kuwataka madiwani hao wasifanye kazi kwa kutetea
maslahi ya watu wachache.
Baraza la Madiwani la
Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza limedaiwa kwamba ni
miongoni mwa mabaraza yanayoongoza kwa mivutano ambayo inadaiwa chanzo
chake ni maslahi binafsi.
Mkurugenzi asusia kikao
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 27, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment