Mmiliki wa klabu ya Fulham, Shahid
Khan, amesema ana tumaini mpango wa kununua Uwanja wa Wembley unaotumika kama
uwanja wa taifa wa England, kutoka kwa Chama cha Soka cha England FA
utakamilika ndani ya wiki nane hadi 12 zijazo
Bilionea huyo mzaliwa wa Pakistani
ambaye ni raia wa Marekani, amesema atalipa kiasi cha £ 900m zaidi ya Shilingi
Trioni mbili kwaajili ya kukamilisha mpango huo. Hata hivyo hajaweka wazi kama
uwanja huo utakuwa ndio uwanja wa Fulham.
''Ninaamini tutakubaliana na FA
ndani ya wiki 8 hadi 12 na biashara itakwenda vizuri kwasababu uwanja
utaendelea kuitwa jina hilo (Wembley), kwa kuheshimu utamaduni wa England
lakini pia timu ya taifa ya England itaendelea kuutumia'', amesema.
Khan mwenye umri wa miaka 67 pia
anamiliki klabu ya Jacksonville Jaguars inayoshiriki katika ligi ya soka la
Marekani (American Football). Ameahidi kama atamiliki uwanja huo timu hiyo
itakuwa na mechi za kirafiki zaidi ya 10 na timu za EPL kila msimu.
Kwasasa Wembley unatumika kama
uwanja wa nyumbani wa Tottenhma Hotspur ambayo ipo kwenye matengenezo ya uwanja
wake mpya unaotarajiwa kukamilika mwaka huu na kuanza kutumika msimu wa
2018/19.
Bilionea kununua uwanja wa taifa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 27, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment