Wabunge
wanaoishi katika maghorofa yanayomilikiwa na Wakala wa Majengo Nchini (TBA)
katika eneo la Area D mjini hapa wamelalamikia uchafu uliokithiri kwenye
majengo hayo
Wakizungumza
leo Jumanne Aprili 24, 2018 katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka 2018/19, mbunge wa viti maalumu (CCM), Mwanne
Nchemba na Joyce Mukya (viti maalumu-Chadema) wamesema uchafu huo umekuwa kero
kwao
Mwanne amesema
maghorofa hayo yamezingirwa na uchafu uliokithiri kutokana na wakala huo
kushindwa kuyafanyia usafi
“Nitoe ushauri
kwa TBA walete waraka maalumu wa kututaka kuchangia angalau Sh10,000 kwa ajili
ya usafi. Wapangaji wana uwezo huo wa kulipa,”amesema
Amesema kwa
sababu kodi wanayotoa ni ndogo wapangaji watoe fedha hizo na TBA watafute
kampuni ya kufanya usafi katika mazingira hayo.
Kwa upande wake, Joyce amesema wapangaji
wamekuwa wakilipa kodi ya pango ya Sh150,000 na Sh250, 000 kwa nyumba moja,
lakini mazingira ya eneo hilo yamegubikwa na uchafu
“TBA haijawahi
kufanya usafi hata wa kupaka rangi katika majengo haya,” amesema.
Amesema
ukarabati unaofanyika katika majengo hayo ni kwa ajili ya nyumba za viongozi
wanaohamia Dar es Salaam.
Wabunge walia kukithiri uchafu nyumba wanazoishi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment