Ndege ya kampuni ya Emirates
iliyokuwa ikielekea Mauritius ikiwa na abiria 475 wakitokea Dubai, imetua
jijini Dar es Salaam leo kwa dharura kutokana na hali mbaya ya hewa nchini
humo.
Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya
Ndege Tanzania, Kamishna msaidizi, Matanga Mbushi amethibitishia taarifa hizo
akisema ndege hiyo ya Emirates, aina ya Airbus 380, EK701, ilishindwa kutua
mara tatu nchini Mauritius kutokana na mvua kali iliyokuwa ikinyesha.
“Hiyo ndege ilikuwa ikielekea
Mauritius, sasa hali ya hewa imekuwa mbaya ikashindwa kutua. Rubani alijaribu
kutua mara tatu lakini akashindwa ndipo akaamua kuja Dar es Salaam kutua kwa
dharura,” alisema Mbushi.
Amesema ndege hiyo ilikuwa na abiria
475 na wote wamepangiwa hoteli ili kusubiri taarifa za hali ya hewa ikiwa nzuri
waendelee na safari.
“Kesho kama hali itakuwa nzuri
wataondoka,” amesema Mbushi.
Ndege hiyo ni ya Shirika la Emirates
la Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE). Ni kampuni tanzu ya Emirates Group,
ambayo inamilikiwa na Shirika la Uwekezaji la Serikali ya Dubai.
Ndege Kubwa Zaidi ya Emirates Iliyobeba Abiria 475 Yatua kwa Dharura Dar
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment