Msanii
nguli wa Bongo Fleva nchini Tanzania, Diamond Platnumz, kwa kushirikiana na
kampuni ya Coca-Cola ametangaza kuwa ameshiriki kuimba wimbo utakaosherehesha
Kombe la Dunia 2018 uitwao Colours.
Wimbo huo uliotungwa na mwanamuziki
Jason Derulo wa Florida, Marekani, Diamond ameshiriki kuweka maudhui ya lugha
ya Kiswahili na umetayarishwa na prodyuza Nahreel kwa kushirikiana na
maprodyuza kutoka nchi nyingine chini ya udhamini wa kampuni ya Coca-Cola.
Akiongea na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam, amesema anayo furaha kupata fursa ya kushiriki kuimba
kuimba wimbo wa mashindano haya makubwa ya kidunia na kuitangaza Tanzania na
lugha ya Afrika bila kusahau tasnia ya muziki kwa ujumla.
“Kwangu hii ni nafasi nyingine
ambayo najivunia kuipata ya kutangaza muziki wa kitanzania sambamba na lugha ya
Kiswahili kwa kuwa sehemu niliyoshiriki kuimba nimetumia lugha ya taifa la
Tanzania ambayo inazidi kupata umaarufu mkubwa duniani”alisema Diamond
Kwa upande wake Meneja wa Chapa ya
Coca-Cola nchini, Sialouise Shayo, alisema kampuni ya Coca-Cola ambayo ni moja
ya mdhamini wa mashindano haya makubwa ya soka duniani inayo furaha kwa msanii
kutoka nchini Tanzania kushiriki kuimba wimbo maalum wa mashindano haya. “Tuna
imani watanzania watapata mzuka wa soka dimbani na kujisikia sehemu ya
mashindano haya”alisisitiza.
Prodyuza nguli wa muziki nchini na
kanda ya Afrika Mashariki, Nahreel ,ambaye ameshiriki kutengeneza wimbo huu
aliishukuru kampuni ya Coca-Cola kwa jitihada mbalimali ambazo imekuwa ikifanya
kuwanyanyua wasanii wa hapa nchini ambapo mbali na Diamond naye ameshiriki
kwenye tukio hili kubwa. “Ninayo furaha ya kufanya kazi na Diamond kwa mara
nyingine katika tukio hili kubwa la mashindano ya Kombe la Dunia na najivunia
heshima kubwa tuliyopewa”
Msanii Diamond Kutoa Burudani Kombe La Dunia 2018 Nchini Urusi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment