Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ameangazia mkataba kati ya Shirika la
Umeme Tanzania (Tanesco) na Songas akishauri ufanyiwe tathmini upya
Katika ripoti
ya ukaguzi wa mashirika ya umma kwa mwaka wa fedha 2016/17, CAG anasema kuna
uwezekano kuwa Tanesco haikupata thamani ya fedha kwa mali zilizohamishiwa
Songas, kiasi kwamba thamani ya hisa ilizopewa shirika hilo zinaweza kuwa za
chini kuliko thamani halisi ya mali hizo
CAG anasema
alibaini eneo la Ubungo Complex lilihamishwa kwenda Songas mwaka 2004 wakati
Songas ilipoanza kufanya kazi zake Tanzania. Kutokana na mkataba wa kuhamisha,
uhamisho huo ulihusisha haki ya umiliki wa ardhi na mali zisizohamishika,
umiliki wa mali zinazohamishika (pamoja na vipuli na injini ya kufua umeme
-turbines), tafiti (intellectual properties) na haki yoyote kutoka kwa shirika
la umeme ambayo itaiwezesha Songas kumiliki, kufanya kazi na kudumisha Ubungo
Complex
CAG anasema
Tanesco ilipewa hisa 10,000 katika mtaji wa Songas na Songas ilichukua madeni
ya Tanesco ambayo yalitumika kununulia injini nne za maji zilizopo eneo la
Complex.
Kutokana na
mkataba wa usimamizi kati ya Jamhuri ya Muungano na Benki ya Biashara ya Ulaya,
mchango wa mtaji wa Tanesco na Shirika la Maendeleo la Mafuta Tanzania (TPDC)
katika Kampuni ya Songas ni Euro 5 milioni, ambapo Shirika la Maendeleo ya
Mafuta lilikuwa na hisa 20,000. “Hata hivyo, kulikuwa hakuna ushahidi
unaoonyesha eneo la Complex na mali zake ambazo zilihamishwa kwenda kampuni ya
Songas zilikokotolewa thamani yake kabla ya kuhamishwa,” anasema
“Pia, hakuna
kipengele katika makubaliano ya kuhamisha na mkataba wa mkopo kinachoonyesha
kiasi cha mkopo uliochukuliwa na Songas uliotumika kununua injini za kufua
umeme
Ripoti
inaeleza mkataba wa usimamizi wa fedha ambao ulisainiwa kati ya Serikali, Benki
ya Biashara ya Ulaya na Songas unaonyesha gharama ya mradi wa Songas ilikuwa ni
Euro 392 milioni (sawa na Dola 346 milioni za Marekani kwa wakati ule).
Hata hivyo,
anasema alibaini Serikali ilifanya uwekezaji mkubwa wa asilimia 73 katika mradi
bila kuuthaminisha
“Hakuna sehemu
yoyote kwenye mkataba ambayo inaonyesha umiliki wa Serikali kwenye mradi licha
ya uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali,” anasema
Alipotafutwa
na Mwananchi kuzungumzia kipengele hicho cha ripoti ya CAG, meneja biashara wa
Songas, Sebastian Kastuli alisema wanazijua taarifa hizo ila hawawezi kuweka
utetezi wao kwenye vyombo vya habari
“Tuna taarifa
hiyo, lakini tungependa kujibu moja kwa moja kwa CAG na kwa Rais, kwa hiyo
tusingependa kueleza kwa vyombo vya habari,” alisema Kastuli.
Akizungumza na waandishi wa habari juzi,
waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani alisema kuna hoja atazijibu bungeni.
Mkataba wa Tanesco, Songas waguswa katika ripoti ya CAG
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment