Watoto wa kike kuanzia umri wa miaka 9-14 kipatiwa Kinga ya saratani ya Mlango wa Kizazi kuanzia Leo Arusha
Jumla ya Watoto wa kike 21198 wenye umri wa miaka 9-14 Mkoani Arusha wanatazamiwa kupata chanjo ya kuzuia Saratani ya mlango wa kizazi ambayo husababishwa na maambukizi virusi vya Papilloma.
Amesema dalili za saratani ya mlango wa kizazi kutokwa na damu bila mpangilio,maumivu ya mgongo,miguu na kiuno kuchoka kupungua uzito,kupungukiwa hamu ya kula,kutokwa uchafu kwenye uke wa majimaji uliopauka wa rangi kahawia au wenye damu na kubimba miguu.
Pamoja na hayo ,Wizara ya Afya mkoani hapa wamevitaka vyombo vya habari kubaini uzushi ama uvumi kuhusu chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi na kutoa taarifa kwa wataalamu wa afya katika mamlaka husika na kutoa mrejesho kwenye jamii baada ya kupata ufafanuzi wa kitaalamu
Mganga Mkuu mkoani Arusha Timothy Wonanji ametolea ufafanuzi wa chanjo hiyo na kusema kuwa ni salama, imethibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) na Mamlaka ya Chakula naDawa Tanzania (TFDA)
Amesema Nchini Tanzania saratani ya mlango wa kizazi ni ya kwanza ,ikifuatia ile ya matiti zote kwa pamoja husababisha vifo kwa asilimia 50 vya kinamama,inaweza kusambaa na kushambulia kibofu cha mkojo,uke na sehemu za chini ya utumbo mkubwa na baadaye figo, ini na sehemu nyingine.
Kwa upande wake Daktari Mwandamizi kutoka TAMISEMI Boniface Mguhuni ameainisha visababishi vya saratani ya mlango wa kizazi kuwa ni pamoja na kujaamiana katika umri mdogo,kuwa na wapenzi wengi,kuwa na ndoa za mitala,kuzaa watoto wengi pamoja na uvutaji wa sigara.
" Mwaka 2018 chanjo itatolewa kwa wasichana waliofikisha umri wa miaka 14 na ili kupata kinga kamili walengwa watahitaji kupatiwa dozi mbili.
Dozi ya pili itatolewa miezi 6 baada ya kupata dozi ya kwanza".alisema Timoth.
Amesema Nchini Tanzania saratani ya mlango wa kizazi ni ya kwanza ,ikifuatia ile ya matiti zote kwa pamoja husababisha vifo kwa asilimia 50 vya kinamama,inaweza kusambaa na kushambulia kibofu cha mkojo,uke na sehemu za chini ya utumbo mkubwa na baadaye figo, ini na sehemu nyingine.
Kwa upande wake Daktari Mwandamizi kutoka TAMISEMI Boniface Mguhuni ameainisha visababishi vya saratani ya mlango wa kizazi kuwa ni pamoja na kujaamiana katika umri mdogo,kuwa na wapenzi wengi,kuwa na ndoa za mitala,kuzaa watoto wengi pamoja na uvutaji wa sigara.
Mratibu wa afya ya uzazi na mtoto mkoani Arusha Belinda Mumbuli amesema mwaka 2017 wanawake 6079 walipimwa Saratani ya mlango wa kizazi mkoani Arusha ,kati ya hao 138 walionekana na dalili za awali ,45 walipewa rufaa kwaajili ya uchunguzi zaidi
Amesema dalili za saratani ya mlango wa kizazi kutokwa na damu bila mpangilio,maumivu ya mgongo,miguu na kiuno kuchoka kupungua uzito,kupungukiwa hamu ya kula,kutokwa uchafu kwenye uke wa majimaji uliopauka wa rangi kahawia au wenye damu na kubimba miguu.
Inakadiriwa kuwa kila mwaka kati ya wanawake 466,000 wanathibitika kuwa na saratani ya mlango wa kizazi na wengi wao wako katika nchi zinazoendelea.
Dkt.Salum Msheshe kutoka ofisi ya mganga mkuu Arusha amewataka wazazi na jamii kuacha kudanganyana na kuzusha mambo ambayo yatakwamisha juhudi za kutolewa chanjo hiyo badala yake wawapeleke watoto wao wakapatiwe chanjo
Pamoja na hayo ,Wizara ya Afya mkoani hapa wamevitaka vyombo vya habari kubaini uzushi ama uvumi kuhusu chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi na kutoa taarifa kwa wataalamu wa afya katika mamlaka husika na kutoa mrejesho kwenye jamii baada ya kupata ufafanuzi wa kitaalamu
Watoto wa kike kuanzia umri wa miaka 9-14 kipatiwa Kinga ya saratani ya Mlango wa Kizazi kuanzia Leo Arusha
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment