Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) limeipa onyo kali vinara wa michuano ya ligi kuu Simba SC
kutokana na kitendo chao kuchelewa kufika uwanjani dakika 6 katika mchezo wa
namba 191 ulichochezwa dhidi ya Mbeya City kwenye dimba la Taifa Jijini Dar es
Salaam Aprili 12, 2018.
Hayo yamebainishwa na taarifa
zilizotolewa na Mtendaji mkuu wa Bodi Ligi Boniface Wambura na kusema Kamati ya
Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi (Kamati ya Saa 72) ya Bodi ya Ligi katika kikao
chake kilichopita kiliweza kupitia taarifa na matukio mbalimbali na kukuta
baadhi ya vitu vikiwa vimetendeka ndivyo sivyo nakuamua kutoa uamuzi wao.
"Kitendo cha Simba ni ukiukaji
wa Kanuni ya 14(9) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo wakati adhabu dhidi
yao imekijita katika Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za
Mchezo", amesema Wambura.
Simba wanatarajiwa kushuka dimbani
Aprili 29, 2018 katika dimba la Taifa Jijini Dar es Salaam kuminyana na watani
wao jadi Yanga katika michuano ya ligi kuu.
Simba yapigwa onyo kali
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 26, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment