"Kamwe hatutamwonea huruma mtu” - Rais Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amesema kwamba serikali zote mbili hazitamvumilia mtu yeyote ambaye ana lengo la kuuvunja Muungano. 

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akihutubia umma uliohudhuria kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kwenye uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.

Rais Magufuli amesema kwamba Muungano ni mali ya Watanzania hivyo ni jukumu la kila mmoja kuulinda, kwani ndio silaha yetu kama nchi.

"Kwanza napenda kurudia kuwakumbusha Watanzania wenzangu kwamba Muungano wetu ndiyo nguvu yetu na ndio silaha yetu, kila mmoja ana wajibu wa kuulinda. Serikali zote mbili za Tanzania Bara na Zanzibar, kamwe hatutamwonea huruma mtu yeyote, awe raia wa hapa nchini au wa nje ya nchi, atakayetaka kuvunja muungano wetu”, amesema Rais Magufuli.

Pia Ras Magufuli amesema kwamba kufikisha miaka 54 ya Muungano sio kitu rahisi na pia ni kitu cha kujivunia, kwani wapo ambao walijaribu kuungana lakini wameshindwa kudumu kwenye muungano huo.






"Kamwe hatutamwonea huruma mtu” - Rais Magufuli "Kamwe hatutamwonea huruma mtu” - Rais Magufuli Reviewed by KUSAGANEWS on April 26, 2018 Rating: 5

No comments: