Baada ya Mwenyekiti wa umoja wa jumuiya ya wanawake mkoa wa Arusha Yasmini Bachu kutembelea soko la Tengeru halmashauri ya wilaya ya Meru na kupata malalamiko kutoka kwa wanawake wafanyabiashara kuhusu kulipishwa kodi mara mbili kwenye soko hilo wilaya hiyo imeshaanza kushughulikia tatizo hilo.
Akizungumza katika mkutano wa Baraza la wanawake halmashauri ya Meru katibu tawala wa wilaya ya Arumeru Mzava amesema kuwa wanafanya
utaratibu wa kuwasilisha amesema kuwa wameshapokea maelekezo kutoka
kwa mwenyekiti huyo na watawasilisha kwake kwa maandishi.
“Niseme tu mwenyekiti tumejipanga vizuri kuhakikisha kwamba maelekezo na miongozo inayotolewa na vikao na viongozi na wa chama inafanyiwa kazi kwa wakati tunajua kwamba mh Mwenyekiti alifanya ziara kwenye masoko yetu alifanya kwenye soko la Tengeru na kule Lokii pamoja na kwamba hatukupata barua lakini tulipoona tu zile video sisi tulianza kufanya kazi na naamini baada ya muda flani utapata majibu ya maandishi kabisa kwamba serikali ya wilaya imefanya nini kwenye changamoto ambazo ulielezwa na wafanyabiashara ulipotembelea maeneo yale tunafanya hivyo kwa kutambua kwamba hiyo ndiyo njia pekee na silaha ya kwanza ya utekelezaji wa Ilani kwa hiyo nikuambie tu mwenyekiti tutakuletea taarifa za maandishi kwamba tumefanyia kazi changamoto hiyo”Alisema Mzava
Hata hivyo mwenyekiti Yasmini Bachu yupo wilaya ya Meru kwa ajili ya Mkutano wa baraza la wanawake ikiwa na lengo la kufanya Zara ya kukutana na mabaraza yote katika mkoa wa Arusha
No comments:
Post a Comment