Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kanda ya kaskazini kimesaini hati ya mashirikiano Matano na chama cha CHADEMA DIASPORA kilichoppo WASHNGTON SEATTLE nchini Marekani lengo likiwa ni kujenga misingi ya chama kupitia maelewano ya kupeana fursa mbalimbali zikiwemo za kibiashara, Masoko , Siasa na jamii zitakazowezesha kuking'oa madarakani chama cha mapinduzi 2020.
Akizungumza na vyombo vya habari jijini Arusha Machi 19, Katibu wa CHADEMA kanda ya kaskazini Amani Golugwa amesema mambo mengine waliokubaliana ni masuala ya uenezi wa chama katika kukabiliana na chaguzi mbalimbali zijazo,ikiwemo masuala ya vipeperushi
Golugwa amesema mashirikiano hayo yamelenga kuimarisha misingi ya chama ndani na nje ya nchi hasa katika nyanja za kiuchumi ,pia kuwaunganisha wafuasi wa chadema waliopo nje ya nchi katika kusafiri pamoja na Utoaji na usambazaji wa habari
Kwa upande wake kiongozi wa chama cha chadema, Diaspora Washngton Seattle nchini Marekani ,Pascal Kikubi amesema mashirikiano hayo ni muhimu sana hasa katika kipindi hiki cha siasa za ushindani
Ameongeza kuwa hapo awali kulikuwa na mashirikiano hafifu huku baadhi ya viongozi wa chadema wakifika Marekani na kutoa Ahadi mbalimbali lakini mwisho wa siku kunakuwa hakuna utekelezaji,jambo ambalo wamekubaliana kutojirudia
Amesema baadhi ya mambo waliokubaliana ni masuala ya kisiasa ,kijamii, kubadilishana usafir
CHADEMA NA UKAWA WASHINGTON WASAINI MIKATABA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 20, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment