Diwani Mwingine Arusha Ajiuzulu Chadema na Kujiunga Ccm

Diwani wa chadema ,Kata ya Kaloleni ,jijini Arusha ,Emanuel Kessy amejivua wadhifa wake na kujiunga na ccm Kwa kile alichodai ni kumuunga mkono rais John Magufuli

Kessy Ambaye Amekuwa akitajwa na chadema kuwa ni miongoni  mwa madiwani wenye mpango wa kukihama chama chao ,Jana machi 19 ,Ametangaza kuachia ngazi usiku wa Manane baada ya mke wake kumtilia ngumu .

Kessy pia amejivua uanachana wa chadema  na kutimkia ccm huku taarifa zikieleza kwamba mke wake alikuwa ni kikwazo kuachia ngazi Kwa mumewe hata hivyo baadaye ilifanikiwa kumrubuniwa na hatimaye ilipofika majira ya usiku alilegea na kukubali mumewe aachie ngazi

Wakati kukiwa na taarifa hiyo iliyofanya idadi ya madiwani wa chadema jijini hapa kutimkia ccm kufikia 6,uongozi wa chadema mkoani hapa umekitupia lawama kikundi cha wanaccm wanaoendesha mpango wa kuwarubuni madiwani wao .


Diwani Mwingine Arusha Ajiuzulu Chadema na Kujiunga Ccm Diwani Mwingine Arusha Ajiuzulu Chadema na Kujiunga Ccm Reviewed by KUSAGANEWS on March 20, 2018 Rating: 5

No comments: