Lusaka, Zambia. Rais Edgar Lungu
ameshtushwa kusikia wanachama wa chama kikuu cha upinzani cha UPND
wanaonunuliwa kujiunga chama tawala cha PF wanalipwa K20,000 na wengine K5000
badala ya kiasi kilichotengwa cha kati ya K200,000 na K500,000.
Haijajulikana chanzo cha fedha
hizo kama ni chama au serikali lakini kiasi kikubwa cha fedha kimeidhinishwa
na rais kwa ajili ya mradi wa kununua madiwani wa chama cha United Party for
National Development (UPND) kinachoongozwa na Hakainde Hichilema.
Lungu alionyesha mshtuko huo
alipozungumza na maofisa waandamizi wa chama tawala cha Patriotic Front (PF)
kwenye Ikulu muda mfupi baada ya kurejea nchini akitokea Afrika Kusini kwa
shughuli binafsi.
Rais alimwambia Davies Mwila
kwamba kila diwani anayehama kutoka UPND alitakiwa kulipwa kiasi kinachofikia
K200,000 wakati wale kutoka kwenye ngome za UPND kama vile jimbo la Kaskazini
Magharibi walipaswa kupewa hadi K500,000.
Katika siku za hivi karibuni
baadhi ya madiwani wa UPND walikiri kuwa wanalengwa kushawishiwa kuhamia PF
baada ya kupewa K20,000 wakati wengine walipewa kiasi kidogo cha K5000
Pia madiwani hao walidanganywa
kwamba wakihamia PF watateuliwa kuwa wakuu wa wilaya au kupewa kazi nyingine
serikalini lakini mpaka sasa hakuna chochote kilichofanyika
“Waungwana, imekuwaje tunajikuta
katika aibu ambapo sasa madiwani UPND wanabadili mawazo yao? Kaizar Zulu
alikuja hapa akaniambia tutekeleze mpango wa kisiasa wa kupata madiwani wa
UPND kote nchini," alisema
i kwamba kila diwani wa UPND
ambaye anakubali kujiuzulu katika maeneo kama Kaskazini, Luapula, Copperbelt,
Mashariki na Muchinga walitakiwa kupewa K200,000 pamoja na kazi ya
maana. Wale wa majimbo ya Kaskazini Magharibi, Magharibi na Kusini
walitengezwa K500,000 kila mmoja pamoja na gari na kazi kwa kuwa tusingeweza
kutetea viti vyetu kule. Tulitaka tu kupima umaarufu wetu katika maeneo yale
“Lakini ni dhahiri fedha
zilizotolewa hazikuwafikia madiwani waliolengwa. Sasa ni nini
kinachoendelea?" alihoji Lungu wakati akiomba kupewa ripoti
kamili."
Maoni ya
Lakini vyanzo kutoka ndani ya PF
vimesema kuna watu kama Kaizar Zulu wanaodhoofisha uongozi wa Edgar Lungu.
Walifichua kwamba Lungu
anadanganywa kwamba ana umaarufu wa kiwango cha juu na yeye anaendelea kutoa
fedha ambazo zinaingia kwenye mifuko ya wale wanaomwona kuwa hawezi kufika
popote
"Kinachotokea ni kwamba ni
wazi kabisa kuwa watu wengine wananufaika na hali hiyo na ukosefu wake wa
ujuzi wa siasa sahihi nchini. Wanamwambia kwamba bado anajulikana sana na
atashinda tena kwa kishindo. Jambo la kushangaza ni kwamba yeye pia
anakiamini kikundi hiki kidogo kinachomzunguka. Lakini kile ambacho hajui ni
kwamba hili ni kundi la wahuni ambao wanajali biashara zao," kilisema
chanzo kutoka PF.
"Kazi yao ni kupora tu
rasilimali za umma hata kutoka kwake na kununua mali zao. Je, unaweza
kufikiri kwamba Rais wetu hakuwa anajua hata kiwango ambacho Rais wa UPND
Hakainde Hichilema ameingia maeneo kama vile majimbo ya Mashariki na
Kaskazini.”
|
Rais Lungu atenga bajeti ya kununua wapinzani Zambia
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 19, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment