"JUMUIYA YA UWT NDIYO KIMBILIO LA WANAWAKE" YASMINI BACHU

Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake mkoa wa Arusha Bi Yasmini Bachu amewasihi akinamama kushirikiana kwa pamoja na ofisi za wanawake wa jumuiya hiyo mkoa kwasababu ndiyo kimbilio la wanawake katika kuisimamia serikali ili kuleta maendeleo.

Bachu ameyasema hayo katika siku yake ya pili ya ziara yake wilayani Meru ya kukutana na mabaraza ya wanawake kwa ajili ya kuzungumza nao na kutoa shukrani kwa kuchaguliwa pamoja na kutoa elimu kwa wanawake kupitia watumishi wa serikali kuhusu haki za wanawake,ujasiriamali na elimu ya uongozi.

Amesema kuwa kwasasa kinachotakiwa ni kuhakikisha jumuiya hiyo inaboreshwa vizuri kwa kutumia nafasi aliyopewa ya kusimamia wanawake ambao kwa muda mrefu hawakuwa na sehemu ya kutoa mawazo yao.

Hata hivyo amesema kuwa moja ya kazi ya jumuiya ni kusimamia serikali na kuhakikisha chama cha mapinduzi kinasimamia serikali na wanashinda chaguzi zote kuanzia serikali za mitaa mpaka taifa.
Ameongeza kuwa kwa kutumia asasi mbalimbali za wanawake kwa ngazi zote wanajadili mambo yanayohusu maendeleo ya wanawake na watoto kwa ujumla.

Kuhusu masuala ya nafasi za uongozi Bachu amesema kuwa watahakikisha wanahamasisha wanawake wanajitokeza kugombea nafasi za uongozi na kufanya mikutano ili kueleza mafanikio ya utekelezaji wa ilani ya CCM kufuta hoja za uongo za upinzani dhiti ya chama tawala.

Awali akitoa taarifa mbele ya mwenyekiti wa UWT Katibu wa jumuiya hiyo wilayani Meru Frida Kaaya amesema kuwa mpaka sasa kuna wanachama 2487 waliolipa ada ni 250 ,na wanachama wapya ni 249 na wanaendelea kuhamasisha wanachama wa zamani kulipa ada zao na kuingiza wanachama wapya hasa wenye umri wa kati.

Frida ameongeza kuwa ni kwa mara ya kwanza kwa mwenyekiti huyo kufanya ziara ambayo imeleta manufaa makubwa kwasababu siku za nyuma aliwahi kuja katika eneo la miradi ya jumuiya tawi la Sing”isi na kuagiza mali za jumuiya ya wanawake ziwanufaishe wanawake wenyewe.

Yasmini Bachu anafanya ziara katika mkoa wa Arusha wa kukutana na wanawake wa wilaya zote za mkoa kwa ajili ya kuzungumza nao kutambua changamoto pamoja na kutoa elimu za ujasiriamali na mpaka sasa ametembelea wilaya mbili za Meru na Arumeru  
"JUMUIYA YA UWT NDIYO KIMBILIO LA WANAWAKE" YASMINI BACHU "JUMUIYA YA UWT NDIYO KIMBILIO LA WANAWAKE" YASMINI BACHU Reviewed by KUSAGANEWS on March 20, 2018 Rating: 5

No comments: