Waziri wa kilimo na
ushirika Dkt. Charles Tizeba amepokea ripoti ya uchunguzi wa sakata la korosho
zilizokutwa na mawe nchini Vietnam kisha kumuagiza katibu mkuu wizara hiyo
kushirikiana na vyombo vya dola kuwakamata na kuwahoji wote waliohusika.
Dkt. Tizeba ametoa agizo hilo mjini
Dodoma baada ya kupokea ripoti ya timu ya uchunguzi aliyounda Februari mwaka
huu kutoka kwa makamu mwenyekiti wa timu hiyo Kassim Mbufu, ili kuchunguza
sakata hilo ambalo limewataja baadhi ya maafisa wa serikali waliosimamia
mchakato mzima wa kusafirisha korosho hizo kuanzia bandari ya Mtwara, Dar es
salaam hadi Vietnam.
Akizungumza wakati wa kukabidhi
ripoti makamu mwenyekiti timu hiyo Kassim Mbufu ameshauri serikali kufanya
mazungumzo na serikali ya Vietnam na kuwaeleza hatua walizochukua ili kuzuia
udanganyifu huo.
Kwa upande mwingine, Waziri Tizeba
ameahidi kufanya mazungumzo na wabunge wa Vietnam wanaotarajiwa kuwasilli
nchini hivi karibuni kwa niaba ya serikali ya nchi yao ili kuwaeleza hatua
walizochukua na jinsi ya kuzuia vitendo hivyo vyenye lengo la kuharibu soko la korosho
ya Tanzania.
Waziri Tizeba aagiza vyombo vya dola kuwakamata waliohusika sakata la Korosho
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 22, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment