MASHINJI ASEMA JESHI LA POLISI WANAWASUMBUA SANA


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia Katibu Mkuu wake Dkt. Vicent Mashinji amesema wanafanyiwa usumbufu na Jeshi la Polisi wa kuitwa kila wiki na mwishowe hakuna jambo jipya wanaloambiwa wanapokuwa wameitikia wito wa kuripoti.

Dkt. Vicent Mashinji ametoa kauli hiyo muda mchache alipotoka nje ya kituo cha Polisi 'Central' Jijini Dar es Salaam leo (Machi 22, 2018) baada ya kuitikia wito wa Kipolisi kama walivyotakiwa kufanya hivyo awali kwa lengo la kuhojiwa juu ya tuhuma za kufanya mkusanyiko usiokuwa halali.

"Jambo moja nataka niwakumbushe watanzania wenzangu kwamba Tanzania tunakitu kinachoitwa kiingereza 'Police Force' hatuna 'Police services' yaani maana yake tuna Jeshi la Polisi la kusukuma watu nasio la kutoa huduma mbalimbali kwa jamii", amesema Dkt. Mashinji.

Pamoja na hayo, Dkt. Mashinji ameendelea kwa kusema "kila bada ya siku tatu nne tunakuja, tunakaa hapa hakuna jambo lolote la maana linalofanyika kwa hiyo inaonekana tu kwamba ni usumbufu tu. Muda mwingine mtu anapoamua kukusumbua tu unampa fursa tu naye ajisikie tu raha afanye kile anachojisikia, kimsingi hakuna jambo lolote tunalolivunja kisheria zaidi ya wao ya usumbufu mara kwa mara. Sisi tutaendelea kuripoti kulingana na wao wanavyotaka".

Kwa upande mwingine, viongozi wa CHADEMA wametakiwa kurudi tena kituo cha Polisi Jijini Dar es Salaam siku ya Jumanne Machi 27 mwaka 2018.

MASHINJI ASEMA JESHI LA POLISI WANAWASUMBUA SANA MASHINJI ASEMA JESHI LA POLISI WANAWASUMBUA SANA Reviewed by KUSAGANEWS on March 22, 2018 Rating: 5

No comments: