Naibu Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson amefunguka na kusema kuwa
yeye hana uhakika kama mwanadada mwanaharakati wa mitandaoni Mange Kimambi kama
ni binadamu wa kawaida kama yeye.
Tulia Ackson amesema hayo
alipohojiwa na moja ya chombo cha habari na kusema kuwa kwa sasa hawezi kusema
kama mwanadada huyo anakosea au laa kwa kuwa hana uhakika kama yupo kama yeye na
kusema labda akipata fursa ya kuonana naye na kuona kweli yupo kama yeye ndiye
anaweza kuwa na la kusema.
"Sina hakika kama yeye ni
binadamu wa kawaida kama mimi kwa hiyo sijui labda nikikutana naye ndiyo
nitajua chakuzungumza naye lakini kwa yale nayoyasikia hapa na pale sina hakika
kama yeye ni binadamu wa kawaida kama mimi ila kama yupo kama mimi basi nitapata
fursa ya kumshauri nikionana naye, siwezi kusema anakosea kama nilivyosema
sijajua yeye ni mtu wa namna gani kwa hiyo huenda hakosei labda ni aina yake ya
binadamu yaani ni specie tofauti hivyo kama yeye ni specie ya tofauti huwezi
kusema anakosea" alisema
Tulia Ackson
TULIA SIAMINI KUWA MANGEKIMAMBI NI BINADAMU WA KAWAIDA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 22, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment