Msanii wa filamu na
mchekeshaji hapa bongo Ebitoke, ameweka wazi juu ya kufufuka kwa penzi lake na
Ben Pol ambaye hapo awali alidai hapokei hata simu zake, na hivi karibuni
kuanza kuwa pamoja tena.
Akizungumza Ebitoke amesema kwamba
kitendo cha yeye kuonekana na Ben Pol kwenye kazi zake za comedy ni kwamba
alishamuahidi kuwa atamsaidia kwenye kazi zake, na si ndumba kama baadhi ya
watu wanavyodai, kutokana kwamba penzi lao lilishakufa.
“Sijamroga Ben Pol, hata hivyo
kipindi cha kati kati ambacho mahusiano yetu hayakuwa sawa, sio kwamba hayakuwa
sawa ni kwamba alinituliza nisiongee sana kwenye mitandao baada ya ile kusema
hapokei simu zangu na kuwa niweze ku-manage mahusiano, tulikaa kama mwezi mzima
tulikuwa hatuongelei chochote, lakini aliniahidi kuwa atanisaidia kazi ndo
hivyo tunasaidiana”, amesema Ebitoke.
Wawili hao bado kuna sintofahamu
kama ni kweli wapenzi, kwani mara nyingi Ben Pol amekuwa sio mtu wa kufurahia
suala la mahusiano yake na Ebitoke kuwa wazi.
Ebitoke afunguka kuhusu kumroga Ben Pol
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 22, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment