Katibu Katibu Mkuu wa Chadema (Bara),
John Mnyika na Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Serengeti, John Heche
wameachiwa kwa dhamana baada ya kuhojiwa kwa zaidi ya saa mbili katika Kituo
Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam
Mara baada ya kuachiwa, Heche
ambaye ni mbunge wa Tarime Vijijini amesema kitendo cha viongozi wa Chadema
kuripoti polisi na kukaa kwa saa tano bila kuhojiwa chochote na kutakiwa
kuripoti siku nyingine ni sawa na kifungo cha nje
“Hii ni mara ya tano ninaripoti
polisi. Polisi Tanzania ni kama wametuhukumu kifungo cha nje, kila baada ya
siku mbili wanataka turipoti kituo kikuu cha Polisi Dar es Salaam bila kujali
unaishi wapi, gharama unazotumia kuja na kurudi Dar es Salaam na
majukumu yako mengine ya kikazi unayoshindwa kuyatekeleza. Kuna wakati
inabidi kukataa uonevu huu,” amesema Heche
Leo Mwenyekiti wa Chadema, Freeman
Mbowe; Katibu Mkuu, Dk Vicent Mashinji; naibu makatibu wakuu, John Mnyika
(Bara) na Salum Mwalimu (Zanzibar) pamoja na Heche waliripoti kituoni hapo
kwa ajili ya mahojiano
|
|
Heche, Mnyika wang’ang’aniwa
polisi, wengine waachiwa kwa dhamana
Hata hivyo, mbunge huyo wa Tarime
Vijijini na Mnyika waliendelea kuhojiwa huku wenzao wakiachiwa kwa dhamana,
sababu ya wao kubaki kituoni hapo ikielezwa kuwa ni kitendo chao cha
kutoripoti Machi 16, 2018
Mara baada ya kuachiwa viongozi
hao wametakiwa kuripoti tena kituoni hapo Machi 27, 2018.
Akizungumza na MCL Digital, Heche
amesema kitendo wanachofanyiwa si sahihi kwa maelezo kuwa baadhi yao ni
wabunge na kwa sasa wanapaswa kushiriki vikao vya kamati za chombo hicho
“Mimi napaswa kuwa katika vikao
vya kamati za Bunge Dodoma. Mbali na hilo nikiwa jimboni kwangu, kutoka huko
mpaka Dar es Salaam natumia nauli zaidi ya Sh1milioni. Hivi kwa nini
hawalioni hili,” amehoji Heche
Amesema kwa hali ilivyo ni vyema
wakaelezwa hatima yao kwa maelezo kuwa mbali na kupoteza fedha, pia
wanashindwa kushiriki shughuli za kibunge
“Mfano wanataka turejee tena
Jumanne ijayo (Machi 27, 2018). Hapa ninaondoka nakwenda Dodoma kushiriki
vikao vya kamati, nitalazimika kuondoka jumatatu ili kuwahi. Sasa huu ni
usumbufu kwa kweli. Katika hili sitakubali nitafanya kitu,” amesema Heche.
Wakili wa viongozi hao, Frederick
kihwelo amesema Mnyika na Heche walizuiwa kuondoka na kutakiwa kuandika
maelezo
"Baada ya kufika,
polisi waliwataka Heche na Mnyika ambao hawakufika Machi 16 . Walitaka
wabaki baada ya wenzao kuondoka na kuwaagiza kuandika ahadi ya maandishi kuwa
Jumanne ijayo watakuwepo,”amesema.
|
HECHE AACHIWA KWA DHAMANA BAADA YA KUHOJIWA KWA MASAA MAWILI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 22, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment