Rais wa Tanzania Dkt.
Magufuli leo amemsihi Waziri wa Ulinzi wa Israel Mhe. Avigdor Lieberman
kumfikishia ujumbe Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kwamba
anamualika nchini Tanzania pamoja na kumuomba kufungua ubalozi nchini.
Rais Magufuli ametoa ombi hilo kwa
waziri wa Israel ammbapo amemfahamisha kwa sasa ubalozi unaotumika ni ule
uliopo Nairobi nchini Kenya.
Aidha Mhe. Rais ametaka makubaliano
ya ushirikiano kati ya Tanzania na Israel katika maeneo mbalimbali yakiwemo
ulinzi na usalama, mafunzo na masuala ya kiuchumi yatiwe saini haraka ili
utekelezaji uanze mara moja.
Pamoja na hayo Rais amemshukuru Mhe.
Lieberman kwa kuitembelea Tanzania na amemhakikishia kuwa Serikali ya Awamu ya
Tano ina dhamira ya dhati ya kuukuza zaidi na kuuimarisha uhusiano na
ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Israel.
Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Balozi wa
Israel hapa nchini Mhe. Noah Gal Gendler, viongozi wakuu wa Jeshi la Ulinzi la
Wananchi Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Polisi.
Kwa upande wake Mhe. Avigdor
Lieberman amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kumkaribisha na kufanya nae
mazungumzo na pia amemhakikishia kuwa Israel imejipanga kuongeza uhusiano na
ushirikiano wake na Tanzania katika maeneo yote ya makubaliano pamoja na
kusaidia kilimo na usindikaji wa chakula.
Magufuli atuma ujumbe kwa Netanyahu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 22, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment