Vijana 2 wamefariki dunia baada
ya kusombwa na mafuriko kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika
eneo la Manolo Zaghati kata ya Lukozi wilayani Lushoto Mkoani Tanga.
Kusaga News ilimtafuta
Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Januari Lugangika simu yake haikupokelewa lakini
Mbunge wa Jimbo la Mlalo Mh Rashidi Shangazi amesema kuwa mvua hizo zimesababisha
uharibifu mkubwa wa Miundo mbinu ya Barabara na Umeme katika jimbo hilo.
Ameongeza kuwa Mvua zimesomba daraja linalounganisha mawasiliano ya jimbo la Mlalo na
Jimbo la lushoto katika eneo la Lukozi na kusababisha mawasiliano kukatika kabisa
na kuleta usumbufu mkubwa kwa wasafiri na wasafirishaji.
Amesema mvua hiyo imeanza Jana majira ya saa 12:30 Jioni Umeme ulikatika karibia
Wilaya nzima baada ya Nguzo zinazopeleka Umeme Lushoto kudondoka katika eneo la
Mji mdogo wa Mombo.
Hata hivyo Mbunge Shangazi amewataka
wananchi wa jimbo lake kuchukua tahadhari ili kuepuka majanga yanayoweza
kujitokeza na ametoa pole kwa maafa hayo yaliyotokea
Jitahidi za kurejesha
mawasiliano zinaendelea baada ya kuwasiliana na wakala wa Barabara nchini
Tanroads
Watu 2 Wafariki Dunia kutokana na Mvua zinazoendelea Kunyesha wilaya ya Lushoto kata ya Lukozi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 11, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment