Rais Dkt. Pombe Magufuli
amesema uwepo wake madarakani ni kutaka kuwatoa watanzania katika shida
mbalimbali walizokuwa nazo na kuwapelekea eneo ambalo watakula raha ili siku
atakapokuja kufa basi hata Mungu ampe nafasi ya kuwaongoza Malaika mbinguni.
Dkt. Magufuli ametoa kauli hiyo
wakati alipokuwa anazungumza na wananchi wa mkoa wa Singida muda mchache kabla
ya kukizindua kiwanda cha mafuta ya Alizeti Mount Meru Millers kilichojengwa
mkoani humo.
"Nataka niwahakikishie
watanzania kuwa mna Rais kweli kweli, jiwe kweli kweli. Sitishwi wala sitishiki
mimi jukumu langu ni kwaajili ya watanzania, nikuhakikisha nawavusha watanzania
kutoka mahali kwenye shida na kwenda mahali kwenye raha. Ninajua hiyo ndio
itakuwa sadaka yangu kwa watanzania ili kusudi hata siku moja nikienda huko
mbinguni Mungu atakaponihitaji, akanichague kutokana na mimi nilikuwa kiongozi
mzuri hivyo unaweza hata kuongoza Malaika polepole kwasababu ninajua kuna
maisha baada ya maisha ya hapa duniani", amesema Dkt. Magufuli.
Pamoja na hayo, Dkt. Magufuli
ameendelea kwa kusema "ndio maana nawaomba sana viongozi wa
dini, masheikh na wale watu mbalimbali katika imani zao tuitangulize Tanzania
kwanza, tusitumike".
Kwa upande mwingine, Rais Dkt.
Maguli amewataka wananchi kufanya kazi kwa bidii ili waweze kujikomboa na
kujiongezea kipato cha maisha.
"Sitishwi wala sitishiki" - Rais Magufuli
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 11, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment