Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ameendelea kuwasisitizia watanzania kuacha kurubuniwa kiakili na baadhi ya watu wasiosihi Tanzania kukubali kufanya maandamano kwa madai watakaothubutu kufanya hivyo hawatapona.
Masauni ametoa kauli hiyo leo (Machi
15, 2018) wakati wa uzinduzi wa vituo sita vya polisi vinavyohamashika katika
Mkoa wa Kipolisi Kinondoni Jijini Dar es Salaam leo na kusema wapo watu
wachache wanaotaka kuwapotosha vijana kuacha kuchangamkia fursa za maendeleo na
kutaka waingie katika maandamano yasioyokuwa na tija ndani yake.
"Katika kipindi hichi wakati
nchi yetu inaelekea katika muelekeo mzuri wa kiuchumi na kwamba agenda nyingi
zilizokuwa kero wa wananchi zimeweza kutatuliwa chini ya uongozi wa awamu ya
tano ila kuna baadhi ya watu waliopo ndani ya nchi na wengine wanaweza kuwepo
nje ya Tanzania ambao ni maadui wa mafanikio ambao wanataka sasa kututoa katika
mstari uliyonyooka kwa kuibua agenda za kipuuzi, kitoto na zisizokuwa za
msingi. Mimi nasema nafasi hiyo hawana", amesema Mhandisi Masauni.
Pamoja na hayo, Mhandisi Masauni
ameendelea kwa kusema "kamwe serikali kupitia Wizara ya Mambo
ya Ndani ya nchi na idara zake zote hatutoruhusu mtu atutoe katika agenda ya
msingi ya maendeleo ya nchi hii kwa kutengeneza vitu vya kipuuzi tu. Kuna mtu
anawataka watanzania waache fursa hizi za elimu, ajira kupitia viwanda
vilivyopo nchini eti wakaandamane. Sasa kama kuna wapuuzi wawili watatu mimi
nasisitiza tu wajaribu na waone.Inapotokea suala la ulinzi na usalama wa nchi
hii, vyombo vyetu vipo imara katika hilo.
Kwa upande mwingine, Mhandisi Hamad
Masauni amewataka watanzania waendelee kuunga mkono Rais Magufuli kwa kuwa nchi
ipo vizuri na inaelekea katika sehemu nzuri.
Watanzania wasikubali kaundamana
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 15, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment