Kamanda wa jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam Tanzania, Lazaro Mambosasa amefunguka na kusema kuwa kama April 26 mwaka huu watu wataandamana kwa mitandao ya kijamii wao hawana tatizo kwa hilo ila kama wataingia barabarani basi wasijute.
Mambosasa amesema hayo wakati akiongea na
kituo cha habari cha kimataifa na kusema kuwa jeshi la polisi limejipanga
kuwadhibiti watu ambao watataka kuvunja sheria za nchi kwa kuandamana
barabarani. Mambo sasa amesema kuwa jeshi hilo limejipanga vizuri hivyo wanawakaribisha
wale ambao watahamisika kuandamana barabarani.
"Ndani ya kanda
mimi nasema hakuna maandamano wanahamasishana wanapotezeana muda na wamezoea
kufanya hivyo na walitishia kufanya hivyo wakati uliopita lakini tunachosema
tumejipanga vizuri sisi ni wasimamizi wa sheria atakayetaka kuvunja sheria
atapambana na sisi lakini asijutie matokeo ya kile atakachokutananacho,
wakiandamana kupitia mitandao ya kijamii manake hakuna tutakaokutana nao
barabarani hivyo wataandamana kwa kuendelea kupeana habari kwenye mitandao na
hilo sisi hatuna shida ndio maana tunaendelea kupuuza yanayopangwa lakini
yoyote atakayehamasika kupitia mtandao akaja barabarani kwa maana ya kuleta
vurugu kuvunja sheria za nchi tutakutana naye tumejipanga"
"Ulinzi upo tu
unataka kujua kiasi gani tumejipanga kwa namna gani? Sisi tupo vizuri katika
hilo na tunakukaribisha barabarani kama unataka kuandamana na wewe" alisisitiza Mambosasa
Mange Kimambi
amekuwa akihamasisha sana watu kupitia mitandao ya kijamii kuandamana katika
siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo kila mwaka sherehe hizo huwa
zinafanyika tarehe 26 mwezi wa nne.
Wakiingia barabarani kuandamana watajuta "Mmambosasa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 15, 2018
Rating: 5
No comments:
Post a Comment