Mwakyembe apongeza hatua ya Baraza la Habari Tanzania, MCT, ya kufungua kesi katika Mahakama ya Afrika mashariki


Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Harison Mwakyembe amepongeza hatua ya Baraza la Habari Tanzania, MCT, ya kufungua kesi katika Mahakama ya Afrika mashariki kupinga Sheria mpya ya Huduma za Habari ya mwaka 2016.


Dk. Mwakyembe amesema, Tanzania ni miongoni mwa nchi 6 Barani Afrika zilizoridhia mkataba wa kuruhusu wananchi wake kuishtaki serikali katika Mahakama ya Kimataifa, na kwamba hatua hiyo inaonesha namna ambavyo wananchi wameanza kutambua namna bora ya kuwasilisha malalamiko yao.

Hivi karibuni Baraza la Habari Tanzania MCT, lilifungua kesi dhidi ya serikali kupinga Sheria mpya ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 kwa madai kuwa inanyima uhuru wa vyombo vya habari.

Awali kabla ya tamko hilo, Dkt Mwakyembe amekutana na mabalozi wa nchi za Marekani na China kujadili namna ya kuhifadhi na kuendesha programu ya kumbukumbu za ukombozi wa bara la Afrika ambayo Tanzania imepewa na nchi za Afrika, kutokana na kuwa kinara katika kusimamia mapambano dhidi ya wakoloni na uhuru wa nchi za Afrika
Mwakyembe apongeza hatua ya Baraza la Habari Tanzania, MCT, ya kufungua kesi katika Mahakama ya Afrika mashariki Mwakyembe apongeza hatua ya Baraza la Habari Tanzania, MCT, ya kufungua kesi katika Mahakama ya Afrika mashariki Reviewed by KUSAGANEWS on March 15, 2018 Rating: 5

No comments: