Mkuu wa
Mkoa wa Morogoro, Kebwe Steven Kebwe amempa wakati mgumu Rais kufuatia ombi
lake la kutaka wananchi ambao wamevamia msitu wa Mvomero kuachwa waendelee na
maisha yao jambo ambalo Rais Magufuli amesema ni kinyume na sheria za nchi.
Rais
Magufuli amesema kuwa anatambua ombi hilo la Mkuu wa Mkoa huyo limekuja baada
ya kuona aliwaruhusu waendelea na maisha yao na kutofukuzwa watu waliovamia
ardhi ya Wizara ya Elimu, wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, iliyotengwa kwa
ajili ya ujenzi wa Chuo.
"Sasa
ule msitu ambao upo karibu na Mvomero pale kumbe nao umeshavamiwa na viongozi
wangu mpo mpaka zimefika nyumba elfu moja na kitu leo mnaniambia nifute ili
kusudi hao watu waendelee kuishi hapo, unajua inaumiza kweli na ombi hili
nimeletewa kwa sababu niliwaruhusu watu wa Kahama kukaa kwenye maeneo yao sasa
wanataka kuichukulia hii kama desturi lakini suala la Kahama lilikuwa tofauti
na suala la hapa, ndiyo maana napata kigugumizi kuvunja sheria ambayo nimeapa kuilinda
lakini Mkuu wa Mkoa ameliomba nitalibebe na kulifanyia kazi" alisema
Magufuli
Aidha
Rais Magufuli alitoa onyo kuwa jambo hilo sasa lisije kuwa mazoea watu kuvunja
sheria kwa makusudi halafu wategemee kutumia kauli ya Rais kupata uhalali wa
jambo hilo na kusema kama watu wakikata mapori yote nchi itakuwa jangwa.
Mkuu wa mkoa ampa wakati mgumu Rais Magufuli
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 15, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 15, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment