Hosptali ya Taifa
Muhimbili MNH imetakiwa kuwa mfano bora wa kuigwa katika kupambana na rushwa
kwa kusimamia haki ya mteja, kutimiza wajibu wa mtoa huduma, maadili ya taaluma
na kutekeleza misingi ya utawala bora.
Hilo limesemwa na Makamu Mwenyekiti
wa Bodi ya Wadhamini ya Hosptali hiyo, Dk Hellen Kondya wakati akizindua rasmi
kamati ya uratibu na kamati ya kudhibiti uadilifu wa hospitali hiyo.
Dk. Kondya amesema ni muhimu kuweka,
uhusiano kati ya majukumu ya kamati hizo na maadili ya kitaaluma ambayo
yamebainishwa vyema katika sheria mbalimbali za taaluma za sekta ya afya.
Naye Mkurugenzi mtendaji wa
Muhimbili, Prof. Lawrence Museru amesema Hosptali hiyo imeunda kamati hizo
ikiwa ni mwitikio wa utaratibu wa serikali unaozitaka idara za serikali na
taasisi za umma kusimamia na kudhibiti uadilifu.
Muhimbili yakabidhiwa majukumu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 15, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 15, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment