Mbunge wa Singida
Mashariki kwa tiketi ya (CHADEMA) Tundu Lissu amefunguka na kuwashukuru
Watanzania kwa maombi yao kwake kufuatia oparesheni nyingine ya 19 ambayo
amefanyiwa katika mguu wake.
Tundu Lissu jana alifanikiwa
kufanyiwa oparesheni hiyo katika mguu wake wa kulia na kuisha salama, madaktari
waliamua kufanya oparesheni hiyo kufuatia kugundua moja ya mfupa wake ulikuwa
ukichelewa kuunga na kudai kuwa kama wasingefanya upasuaji na kurekebisha mfupa
huo ungeweza kuchelewa zaidi na kuja kuvunjika baadae.
"Ninawashukuru kwa sala na
maombi yenu" aliandika
Tundu Lissu kupitia mtandao wake wa Instagram
Hata hivyo Watanzania mbalimbali
wameendelea kumuombea Tundu Lissu ili aweze kupona haraka na kurudia tena
katika hali yake ya zamani ili aweze kurudi nyumbani Tanzania na kuendelea na
majukumu yake ya kila siku.
Tundu Lissu alishambuliwa kwa risasi
mnano Septemba 7, 2017 na watu wasiojulikana akiwa mjini Dodoma na kisha baadae
kupelekwa nchini Kenya kwa matibabu ambapo huku alifanyiwa oparesheni kadhaa
katika mwili wake na baadae alikwenda nchino Beljium kwa matibabu zaidi ambapo
jana amefanikiwa kufanyiwa oparesheni ya 19.
Tundu Lisu Awashukuru Watanzania baada ya Oparesheni yake ya 19.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 15, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 15, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment