Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amekiri kuwa wingi wa watanzania
waliopo nchini ni sauti tosha ambayo inaweza kufanya mambo ya kimaendeleo
katika sehemu mbalimbali bila ya kuwekewa vizuizi.
Dkt. Magufuli ametoa kauli hiyo leo
(Machi 14, 2018) wakati alipokuwa anaweka jiwe la msingi msingi wa ajili ya
ujenzi wa reli ya kisasa ya 'Standard Gauge' katika eneo la Ihumwa, Dodoma na
kuwataka watanzania waendelee kuzaana zaidi ili wazidi kuchapa kazi nchini.
"Tanzania tuna bahati sana
kutokana na ukubwa wa nchi yetu, hivi karibuni tumeambiwa tumefika milioni 55.
Wapo waliosema kwanini milioni 55 tunazana mno, mimi nasema tuzaane zaidi kwa
maana mnapokuwa wengi mnakuwa na sauti hata kwenye 'block' mlizonazo. Idadi ya
watu wetu ni sauti tosha katika Jumuiya ya Afrika Mashariki tunachotakiwa ni
sisi watanzania tuchape kazi", amesema
Rais Magufuli.
Pamoja na hayo, Dkt. Magufuli ameendelea
kwa kusema "suala sio kuwa wengi ila ni namna gani watanzania
waliokuwa wengi watashiriki katika kuleta maendeleo ya nchi yao. Nchi ya
Denmark ina watu milioni 5 lakini kwasababu ya uchapakazi wao wamekuwa wakitoa
msaada mpaka kwenye nchi kama Tanzania yenye watu milioni 55".
Kwa upande mwingine, Rais Dkt.
Magufuli amewataka watu wafanye kazi wasibabiike na uwingi wao kwa maana hata
kama wangekuwa wapo jumla ya watu milioni 1 halafu hawafanyi kazi basi
wataendelea kulia tu suala la njaa pamoja na vyuma kubana.
Watanzania Tuzaane tu maana mnapokuwa wengi mnakuwa na sauti- Rais Magufuli
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 14, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment