Jeshi la Polisi mkoani
Mwanza limewakamata viongozi wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) na wafuasi wake sita kwa tuhuma za kufanya mkusanyiko wa kisiasa
zaidi ya watu 200 bila ya kuwepo na kibali maalumu cha kufanya hivyo.
Hayo yameelezwa na Kamanda wa Polisi
mkoani humo, DCP Ahmed Msangi wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa
habari leo ofisini kwake na kuwataja watu hao kuwa ni Deus Lucas diwani wa kata
ya Mabatini chadema, Daniel Mongo Mwenyekiti chadema tawi la Kiloleli B',
Laurence Chilo, Lameck Kaunda.
Wengine ni Jackson Madebe, Bi
Secilia Butuko, Mwita Sagali na Selemani Gabriel ambapo wote hao walikamatwa
Machi 13, 2018 majira ya saa 10:30 jioni ndani ya nyumba ya Laurence Chilo
wakiwa wamefunga bendera za chama chao na kuweka spika za matangazo huku
wanachama hao wakidai walikwenda kuhani msiba wa mwanachama mwenzao aliyefiwa
na mama yake mzazi miezi sita iliyopita.
Aidha, Kamanda Msangi amesema katika
tukio hilo wameweza kupata bendera ya Chadema, kadi za chama hicho
zilizoandikwa majina nusu na nyingine hazijaandikwa majina, mihuli miwili,
karatasi tatu zenye majina ya mahudhurio na T-shirt zenye nembo ya Chadema.
Kwa upande mwingine, DCP Msangi
amesema Jeshi la Polisi lipo katika upelelezi na mahojiano dhidi ya watuhumiwa
hao na uchunguzi ukikamilika watafikishwa mahakamani.
Viongozi wa CHADEMA wakamatwa na Jeshi la Polisi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 14, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment