Baada ya mtu mmoja
kujificha katika hoteli ya Manadalay Bay na kuwafyatulia risasi kwa dakika 10
watu waliokuwa wakielekea katika tamasha , na kuwaua makumi ya watu huku mamia
wakijeruhiwa , rais Trump alielekea Vegas na kukutana na familia, mashahidi ,
maafisa wa matibabu na huduma za dharura.
Aliondoka katika ndege
ya Air Force One akihisi kwamba siku ilikwisha ilivyokuwa kutokana na hali
iliokuwepo.
Lakini muda mfupi tu
baada ya kuwasili mjini Washington ,hisia zake zilibadilika mara moja.
Na kulikuwa na sababu mbili.
Ziara yake ya Vegas
haikutangazwa katika runinga kadhaa. Lakini ya pili ni kwamba habari kuu
ilikuwa inasema kuwa Rex Tillerson alikataa kukana kwamba alimuita Donald Trump
'Mjinga'.
Waziri wa maswala ya
kigeni alikuwa katika mkutano katika idara ya ulinzi wakati alipotoa tamko hilo
kuhusu rais Trump. Hayo ndio maswala ambayo huwezi kuyafutilia mbali kwa
urahisi.
Huyu ni rais ambaye
anayapatia kipau mbele maswala yote yanayokumba serikali yake hivyobasi tangu
wakati huo 'chuma cha Tillerson kilikuwa kimotoni'.
Ni watu wawili ambao
hawalingani kibiashara licha ya kuwa wote wamekuwa wafanyibiashara wakubwa.
Trump amekuwa akifanya biashara za malkia wa Urembo huku Tillerson
akishughulikia biashara za mafuta na kemikali. Lakini ,mbali na hilo wamekuwa
watu wawili tofauti .
Ni aliyekuwa waziri wa
maswala ya kigeni wa zamani Condoleezza Rice aliyempendekezea bwana Trump, Rex
Tillerson na aliyekuwa mkurugenzi wa Ujasusi CIA Robert Gates.
Walidhani ana uzito na
uzoefu wa kufanyia kazi kampuni kubwa ya Exxon na mtu atakayewakilisha maslahi
ya Marekani na kuitetea kote dunini.
Na wakati wote huo
hakuonekana kuwa mkakamavu katika kazi yake.
Mkutano wake wa kwanza
na vyombo vya habari na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov ulifanyika vizuri huku
wote wawili wakionekana kuwa wakakamavu na mawaziri wasiopenda mchezo.
Na alikuwa na mangi ya
kuogopesha huku akipunguza matumizi ya wizara hiyo bila mkakati wa kuidhinisha
mipango yake.
Idara ya maswala ya
kigeni ya Marekani ilikuwa imekosa mwelekeo huku wafanyikazi wa vyeo vya chini
wakijipatia majukumu makubwa kwa kuwa vyeo vya juu vilikuwa havina maafisa
walioajiriwa.
Ilikuwa hali ya kukosa
mwelekeo. Na baadaye kulikuwa na Donald Trump. Wacha tamko la mjinga - hawa ni
watu wawili ambao hawakuelewana kibinafsi na pia kisera.
Mara kadhaa rais Trump
alimpuuza waziri wake wa maswala ya kigeni. Kuhusu Korea Kaskazini ,rais Trump
alichapisha ujumbe katika mtandao wa Twitter kwamba Tillerson alikuwa akipoteza
muda wake.
Kuhusu maswala mengine
alituma watu wa familia yake kwenda kufanya majadiliano ughaibuni. Kulikuwa na
hisia kwamba Rex Tillerson alikuwa afisini lakini hakuwa na uwezo.
Alionekana kama afisa
ambaye hakuambatana na kazi yake , akisafiri duniani kwa kutumia cheo dhana ,
lakini hakuwa na ushawishi wowote wa kubadilisha fikra za rais.
Hadharani alijionyesha
kuwa mwaminifu na kufanya kazi kana kwamba alikuwa akijua kilichokuwa
kikiendelea wakati ambapo ilikuwa kinyume na yaliokuwepo.
Isipokuwa jana usiku,
alipokuwa akirudi nyumbani kutoka ziara ya Afrika, alikuwa kama kawaida .
Alizungumzia kuhusu kile kilichotokea Salsbury Uingereza ambapo jasusi wa Urusi
na mwanawe wa kike waliwekewa sumu ya kuharibu neva kutoka Urusi.
Mahala ambapo Ikulu ya
Whitehouse haikutoa lawama zozote kuhusu Urusi , Tillerson aliingilia kati .
Pengine aligundua kwamba 'chuma chake kilikuwa kweli motoni' pengine hakujali
tena na alipokuwa katika ndege akafutwa kazi.
Walikuwa watu wenye
hasira za viwango tofauti ,tabia na mitindo ya kutekeleza wajibu wao. Tillerson
aliwasili katika uwanja wa ndege wa kambi ya jeshi ya Andrews ambapo mfanyikazi
wake mmoja alimuelezea kwamba rais Trump amechapisha ujumbe katika mtandao wake
wa Twitter kwamba amefutwa kazi.
Kwa sababu Tillerson
hayuko katika mtandao wa Twitter , ujumbe huo ulilazimika kuchapishwa. Na
majibu ya Trump alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari mapema alfajiri
alisema: Nadhani Rex atafurahi sana... sasa nina hakika.
Orodha ya maafisa wa serikali ya Marekani waliofutwa kazi na
rais Donald Traump au wakajiuzulu tangu achukue mamlaka.
1. Rex Tillerson, waziri wa maswala ya kigeni -
13 Machi 2018
2. Gary Cohn, Afisa mkuu wa maswala ya kiuchumi -
6 Machi 2018
3. Hope Hicks, MKurugenzi wa mawasiliano Ikulu ya
Whitehouse - 28 Februari 2018
4. Rob Porter, Katibu katika Ikuku ya White
House- 8 Februari 2018
5. Andrew McCabe, Naibu mkurugenzi shirika la FBI
- 29 Januari 2018
6. Tom Price, Waziri wa afya - 29 Septemba 2017
7. Steve Bannon, Afisa mkuu wa mipango - 18
Agosti 2017
8. Anthony Scaramucci, Mkurugnzi wa mawasiliano -
31 Julai 2017
9. Reince Priebus, Afisa mkuu wa wafanyikazi wa
umma - 28 Julai 2017
10.
Sean Spicer, Waziri wa
habari - 21 July 2017
11.
James Comey,
Mkurugenzi wa shirika la FBI - 9 Mei 2017
12.
Michael Flynn, Mshauri
wa maswala ya usalama - 14 Februari 2017
13.
Sally Yates, acting
attorney general - 31 January 2017
14.
Preet Bharara, New
York federal prosecutor - 11 March 2017
15.
Paul Manafort, Trump
campaign manager - 19 August 2016
Mada zinazohusiana
Sababu zilizomfanya Trump kumpiga kalamu Rex Tillerson
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 14, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment