Wakili wa viongozi wa
Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Reginald Martine amesema wateja wake
wameitwa kuhojiwa na mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) ili
kutoa ushahidi wa tukio la ‘kutekwa’ kwa mwenyekiti wao, Abdul Nondo.
Akizungumza leo Machi 14, 2018,
Martine amesema tayari viongozi wawili kati ya wanne wa mtandao huo
wameshatoa ushahidi wao, kwamba hakuna vitisho vyovyote walivyopewa na
polisi.
Amesema kuwa polisi wamemhakikishia
kuwa hawatawashikilia viongozi hao na mara watakapomaliza kutoa ushahidi
wataruhusiwa kuondoka
“Utaratibu wa wakili mtu anapokuwa
anatuhumiwa lazima uwe na mteja wako wakati anapohojiwa lakini kama mteja
anatoa ushahidi wakili siyo lazima awepo hivyo wanaendelea kutoa ushahidi
muda,” amesema
Amesema walishauriana na
mmoja wa makamishna kuwa yeye asiwepo na viongozi hao wakati wanatoa ushahidi
wao.
Viongozi wawili mtandao wa
wanafunzi wahojiwa
Waliofika kuhojiwa na DCI ni
mkaguzi wa haki za binadamu, Alphonce Lusako; katibu wa mtandao huo, Malekela
Brigthon; ofisa habari Hellen Sisya na mkurugenzi wa Idara ya sheria, Paul
Kisabo.
Waliokwisha hojiwa mpaka kufikia
leo saa 7 mchana ni Lusako na Brigthon.
|
|
Wakili wa viongozi mtandao wa wanafunzi Wahojiwa na DCI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 14, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment