Dar es Salaam. Mwanajeshi MT
109795 Private Ramadhan Mlaku (28) amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu akikabiliwa na shitaka la mauaji ya askari mwenzie, MT 79512 SGT
Saimon Munyama.
Mshtakiwa huyo alifikishwa
mahakamani hapo leo Jumatano Machi 14, 2018 saa tano asubuhi na gari la
kubebea wagonjwa.
Alishushwa katika gari hilo akiwa
juu ya kitanda cha wagonjwa na kupelekwa chumba cha mawakili wa Serikali
ambapo alisomewa shtaka linalomkabili.
Akisomewa shtaka mbele ya
Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wakili wa Serikali, Mosii Kaima amesema
mtuhumiwa huyo anadaiwa kufanya kosa hilo Oktoba 30, 2017.
Imedai kuwa mshtakiwa ambaye ni
mwanajeshi wa kambi ya Jeshi Makongo siku hiyo akiwa Makao Mkuu ya JWTZ
Upanga, Dar es Salaam alimuua askari mwenzie MT 79512 SGT Munyama.
Baada ya kusomewa shtaka hilo,
mshtakiwa huyo hakuruhusiwa kuongea chochote kwa sababu Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo.
Pia kosa hilo hakuna dhamana kwa
mujibu wa sheria.
Upande wa mashtaka ulidai kuwa
upelelezi bado haujakamilika na Hakimu Simba aliutaka upande wa mashtaka
kujitahidi kukamilisha upelelezi wa kesi hiyo mapema.
Kesi imeahirishwa hadi Machi 28,
2018 kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika
ama la
Baada ya kusomewa shtaka hilo
mshtakiwa huyo alipandishwa tena katika gari la wagonjwa na kurudishwa
mahabusu.
|
ASKARI ALIYEUWA MWENZAKE APANDISHWA KIZIMBANI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 14, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment