Dar es Salaam. Wakili wa viongozi
wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Reginald Martine amesema
wateja wake wameitwa kuhojiwa na mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai
(DCI) ili kutoa ushahidi wa tukio la ‘kutekwa’ kwa mwenyekiti wao, Abdul
Nondo.
Akizungumza leo Machi 14, 2018,
Martine amesema tayari viongozi wawili kati ya wanne wa mtandao huo
wameshatoa ushahidi wao, kwamba hakuna vitisho vyovyote walivyopewa na
polisi.
Amesema kuwa polisi
wamemhakikishia kuwa hawatawashikilia viongozi hao na mara watakapomaliza
kutoa ushahidi wataruhusiwa kuondoka
“Utaratibu wa wakili mtu anapokuwa
anatuhumiwa lazima uwe na mteja wako wakati anapohojiwa lakini kama mteja
anatoa ushahidi wakili siyo lazima awepo hivyo wanaendelea kutoa ushahidi
muda,” amesema.
Amesema walishauriana na
mmoja wa makamishna kuwa yeye asiwepo na viongozi hao wakati wanatoa ushahidi
wao.
|
Viongozi wawili mtandao wa wanafunzi waitwa na DCI Kuhojiwa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 14, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment