Aliyekuwa mbunge wa
jimbo la Laikipa Mshariki nchini Kenya Mathew Lempurkel, amekamatwa tena na
polisi nchini humo, baada ya kuachiwa siku ya tarehe 12 machi, kwa tuhuma za
kupanga mauaji.
Kwa mujibu wa Polisi wa Laikipa
Kaunti Kamanda Simon Kipkeu, bwana Lempurkel ambaye alikuwa mbunge kupitia
chama cha ODM, atafikishwa mahakamani baada ya wapelelezi kukamilisha taarifa
zao.
Lampurkel alikamatwa baada ya
kutishia kukichoma moto kituo cha polisi cha Rumuruti, kwa lengo la kumtoa
mtuhumiwa ambaye alikuwa mahabusu mwezi Julai, 2016.
Mahakama iliamua kuwa Lampurkel ana
kesi ya kujibu juu ya vurugu alizofanya, na kisha kukamatwa tena kwa tuhuma za
kupanga njama hizo za mauaji.
Mbunge akamatwa kwa kupanga mauaji
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 14, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment