WABUNGE WATEMBELEA MGODI WA SEKENKE

Wabunge wanaounda Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira wakiongozwa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Kangi Lugola wametembelea mgodi wa Sekenke one Mkoani Singida na kutoa maagizo.


Katika ziara hiyo kwenye mgodi wa Sekenke uliopo wilayani Iramba Singida, Waziri Lugola ametoa maagizo kwa watendaji wa wilaya hiyo kusimamia vyema sheria za mazingira ili kukabaliana na athali zinazoweza kutokea.

Aidha Waziri pia amewaasa wananchi wanaofanya shughuli mbalimbali za uchimbaji katika mgodi huo kuzingatia utunzaji wa Mazingira kwani bila mazingira kuwa bora hata hizo shughuli za uchimbaji zitasimama.
Kwa upande mwingine Wabunge wanaounda Kamati hiyo wamepata fursa ya kujionea shughuli za uchenjuaji wa dhahabu kwa kutumia zebaki kwenye mgodi huo wa Sekenke one uliopo Kijiji cha Nkonkilangi, Kata ya Ntwike, Tarafa ya Shelui.

Nao wachimbaji wadogo wa madini mgodini hapo pamoja na Afisa Uhamiaji wa Wilaya ya Iramba Bw. Dotto Roman Selasini  wameahidi kuzingatia usafi na kutunza mazingira kwa faida zao na kizazi kichajo.
WABUNGE WATEMBELEA MGODI WA SEKENKE WABUNGE WATEMBELEA MGODI WA SEKENKE Reviewed by KUSAGANEWS on March 17, 2018 Rating: 5

No comments: