Makonda aanzisha Mashindano ya kukimbia

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema anaratibu kuanzisha mashindano ya kukimbia kwa vikundi vya Jogging Club vilivyopo katika Jiji lake ili kunusuru vijana hao wasiweze kujiingiza katika vishawishi vya wizi kutokana na wengi kukosa kazi

Paul Makonda ameeleza hayo leo (Machi 17, 2018) wakati wa ghafla ya uzinduzi wa kazi za kutangaza utalii katika Jiji la Dar es Salaam na kusema amegundua kuwepo kwa vikundi vingi vya vinavyofanya mazoezi ya kukimbia katika nyakati za asubuhi lakini jambo la kushangaza vijana hao wengi hawana kazi za kufanya pindi wanapokuwa wamemaliza kufanya mazoezi hayo.

"Vijana wengi wa 'Jogging Club' hizo wanafanya mazoezi asubuhi halafu hawana kazi za kufanya wanarudi vijiweni, hiyo salama maana unaweza ukashangaa wakajikuta wameanza kuwa na 'speed' kubwa na matokeo yake wakapita na mikoba ya wakina mama kama hawana kazi za kufanya. Kwa hiyo sisi tunaratibu na kupitia hadhara hii niwaambie wananchi kwamba tunapanga mipango kwa kila mwisho wa mwezi kuwepo na mashindano 'Jogging Club",amesema Makonda.

Pamoja na hayo, Paul Makonda ameendelea kwa kusema "kila 'Jogging Club' itakayofanikiwa kuongoza itapewa zawadi ya Milioni 10 kama mtaji wa kuanza kufanya shughuli za kujiendesha kiuchumi katika makundi hayo na tunaanza na wilaya ya Temeke kwa kuwa ndio inayoongoza kwa 'Jogging Club' katika Mkoa wa Dar es Salaam. kwa hiyo tutaifanya mwezi ujao na 'Jogging Club' zote za mkoa tutaku
Makonda aanzisha Mashindano ya kukimbia Makonda aanzisha Mashindano ya kukimbia Reviewed by KUSAGANEWS on March 17, 2018 Rating: 5

No comments: