Waziri wa Afya awataka watumishi kuepuka Rushwa

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu amepiga marufuku wafanyakazi wa idara ya Afya kushiriki kwenye vitendo vya rushwa.

Ummy amebainisha hilo leo kwenye katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo kilichofanyika jijini  Dar es salaam ili kujadili mustakabari wa utoaji huduma za Afya nchini. 

“Marufuku Watumishi wa sekta ya afya nchini kujiingiza kwenye vitendo vya rushwa na kama wapo naomba waache mara moja kwani atakayebainika sheria itafuata mkondo wake mara moja” amesema.

Aidha Waziri Ummy amewaasa watumishi wa sekta hiyo kuwa mfano wa kuigwa haswa katika sehemu ya kutolea huduma za afya wanatakiwa kuwa na lugha nzuri kwa wananchi pindi wanapotoa huduma sehemu zao za kazi.


Naye Mwakilishi wa Katibu Mkuu Taifa wa Balaza la Wafanya kazi TUGHE Bw. Nsubisi Mwasandende amesema  ili kutatua changamoto za magonjwa mbalimbali watendaji wa Wizara ya Afya wanatakiwa kuzingatia upatikanaji wa chanjo.
  
Waziri wa Afya awataka watumishi kuepuka Rushwa Waziri wa Afya awataka watumishi kuepuka Rushwa Reviewed by KUSAGANEWS on March 17, 2018 Rating: 5

No comments: