Dkt Jesse Huwezi kumuondoa mwanasiasa kwenye suala la Mchakato wa Katiba Mpya

Mhadhiri wa somo la Sheria kutoka Chuo kikuu cha Dar es salaam Dkt James Jasse amesema kuwa katika mchakato wa suala la katiba mpya huwezi kumuondoa mwanasiasa kwasababu inagusa moja kwa moja masilahi yake.

Dkt Jesse amesema hayo katika mafunzo kwa wanahabari yaliyoandaliwa na kituo cha Sheria na Haki za Binadamu LHRC juu ya elimu kuhusu sheria na mchakato wa katiba mpya pamoja na haki za binadamu yaliyofanyika mkoani Dodoma.

Amesema kuwa suala hilo kwa kuwa linagusa maslahi ya viongozi moja kwa moja ni vyema na wananachi wakahusishwa katika mchakato huo kwasababu utaepuka malalamiko.

Ameongeza kuwa suala hilo la mchakato wa katiba pia endapo litafanikiwa litasaidia kuleta mgawanyo wa Madaraka, mamlaka , mahusiano na miiko ya viongozi,na namna ya kuweka ukomo wa uongozi pamoja na kufanya ukomo wa madaraka katika mamlaka zao.

Pamoja na hayo Dokta Jesse amesisitiza kuwa suala la mchakato wa katiba siyo la chama au mtu binafsi bali ni kwa ajili ya maslahi ya taifa kwa ujumla hivyo ni vyema jambo hilo kuwa endelevu.
Dkt Jesse Huwezi kumuondoa mwanasiasa kwenye suala la Mchakato wa Katiba Mpya Dkt Jesse Huwezi kumuondoa mwanasiasa kwenye suala la Mchakato wa  Katiba  Mpya Reviewed by KUSAGANEWS on March 17, 2018 Rating: 5

No comments: