Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar Zuberi Katwila, amesema kiwango cha timu yake na wapinzani wao wa hatua ya robo fainali ya kombe la shirikisho Azam FC vipo sawa hivyo wanafanya maandalizi ya kawaida.
“Kwa kawaida kwenye soka hakuna mechi rahisi lakini hatuna hofu na Azam kwani tumekutana nao mara kadhaa tunafahamu aina ya mchezo wao, kikubwa ni kuhakikisha vijana wanakuwa makini ili tupate ushindi na kusonga mbele'', amesema.
Majibu ya Katwila yamekuja punde baada ya timu ya Azam FC kutangaza kuanza maandalizi rasmi kwaajili ya mchezo huo ambao ni muhimu kwa timu zote mbili ili kusaka nafasi ya kuiwakilisha nchini Kimataifa.
Mtibwa na Azam zinatarajia kukutana kwenye mechi hiyo ya robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho nchini ambayo bingwa wake huwakilisha taifa kwenye michuano ya kimataifa. Mchezo utapigwa katika Uwanja wa Azam Complex, Machi 31, mwaka huu.
Mtibwa Sukari wasema hawana wasiwasi Kesho
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 17, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment