Mhadhiri wa Chuo Kikuu udsm Ampa Raisi Magufuli Mbinu ya Kupata Katiba Mpya

Mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es salaam Dkt James Jasse amemshauri Raisi wa jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Dokta John Magufuli kutumia njia ya kuunda kamati ya wataalamu ambayo haifungamani na upande wowote kukaa ili kuona jinsi ya kupata katiba mpya.

Akitoa semina iliyoandaliwa na kituo cha Sheria na haki za Binadamu LHRC  kwa waandishi wa habari wa radio za jamii mkoani Dodoma Dokta Jesse amesema kuwa Njia ya Kutumia Kamati ya Wataalamu gharama yake ni
ndogo kuliko kuitisha tena upya Bunge la Katiba
Katika mafunzo hayo yalioyokuwa yanajenga uelewa kwa wanahabari kuhusu sheria ,haki za binadamu na mchakato wa katiba mpya pamoja na yaliyofanyika mkoani humo amesema suala la katiba ni muhimu kwakuwa ni jambo ambalo litatumika katika vizazi vingine pia.

Amesema kuwa kamati hiyo itakuwa na faida kubwa kwasababu itaangalia kilicho bora kwa kuzingatia Sera za Nchi pamoja na kupewa Hadidu za
Rejea ambapo pia nchi ya keyaa walitumia njia hiyo ya kamati maalum.

“Hii Kenya walifanya baada ya kuwa kuna draft ile ya wananchi unadraft ile ya serilaki wakatengeneza commete of expart wakawambia sasa nyie
tunawapa hadidu za rejea muangalie mazuri yaliokopande zote mtutengenezee draft nzuri halafu tutaipeleka kwa wananchi kwa hiyo wale wana harmonize na kureconsile rasimu ya warioba na katiba
inayopendekezwa na hata katiba hii ya 1977 itakuwana document mbayo itakuwa ni high Brid ina pande zote lakini hili nalo litakuwa ni utashi na nadhani hii ni approach ambayo nadhani Raisi wetu ataipenda na itapunguza garama yake itakuwa ndogo”Alisema Dkt Jesse

Ameongeza kuwa namna ya kuipata kamati hiyo ya wataalamu hao ni kuchagua watu wasioegemea upande wowote na wajiite jina ambalo
wanaweza kutumia katika mchakato huo ili kuwapeleka wananchi kwenye kura ya maoni na kuipitisha kwa kuikubali au kuikataa baada ya kushirikisha rasimu za katiba zote.
Naye afisa msaidizi kutoka kitoka kituoa cha sharia na haki za binadamu waliowezesha mafunzo hayo amesema kuwa wameamua kuchagua
radio jamii kwasababu ndizo zinazosikilizwa zaidi na watu wa vijijini ili kupata uelewa juu ya mchakato wa katiba mpya.

Amesema kuwa watu wengi walioko vijijini hawajui masuala ya sharia na katiba lilikuwa ni jambo ambalo linapotea kwenye masikio ya watu hivyo
wakaona ni vema kuibua kupitia waandishi wa habari ambao wanawagusa wananchi moja kwa moja

Akizungumza meneja wa Radio ya Unyanja Fm Patrick Kosima amesema kuwa wao kama wanahabari semina hiyo wamepata ufahamu na watapata fursa ya
kuandaa vipindi mbalimbali ambavyo vinahusu katiba kwa kuwa wametambua sualala mchakato wa huo ni wapi ulikwama ili waanze kutoa ufahamu kwa
watu wengine

Pia Kosima ameishauri serikali ichukue nafasi yake juu ya kuelimisha wananchi juu ya umuhimu wa mchakato wa katiba mpya kwa kuwa kwasasa
imekaa kimya licha ya kwamba kuna mambo mazuri yanafanyika lakini siyo mbadala wa katiba mpya.

Kwa upande wake Ashura Mohameni Mwandishi wa habari kutoka Radio 5 Arusha amesema kuwa kupitia mafunzo hayo yamewasaidia kupata uelewa wa
namna ya kusaidia wananchi kuhusu katiba naye Paulina Mpiwa kutoka Baloha Fm amesema kuwa yeye alikuwa anashindwa ataanzia wapi lakini kwasasa atajua jinsi ya kuongelea suala hilo.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu udsm Ampa Raisi Magufuli Mbinu ya Kupata Katiba Mpya Mhadhiri wa Chuo Kikuu udsm Ampa Raisi Magufuli Mbinu ya Kupata Katiba Mpya Reviewed by KUSAGANEWS on March 17, 2018 Rating: 5

No comments: